#109
Niwe karibu nawe
Izindi
Couplet 1
{Niwe karibu Nawe, Ee, Mungu wangu, hata katika taabu niwe karibu;} x2 {Huu wimbo wangu, Bwana: Niwe karibu Nawe} x2, {Niwe karibu Nawe, karibu Nawe, Ee Mungu wangu.} x2
Couplet 2
{Ninasafari hapa, sitakawia; Gizani duniani, raha haiko;} x2 {Hata ni hivi, Bwana, niwe karibu Nawe} x2, {Niwe karibu Nawe, karibu Nawe, Ee Mungu wangu!} x2
Couplet 3
{Hata mateso mengi yananipita, nitakumbuka hili, Una Rehema,} x2 {Na yatanikokota niwe karibu Nawe} x2, {Niwe karibu Nawe, karibu Nawe, Ee Mungu wangu!} x2
Couplet 4
{Saa nitakapokwenda kwako Mbinguni, nitasahau taabu ya duniani,} x2 {Ungali wimbo wangu: niwe karibu Nawe} x2, {Niwe karibu Nawe, karibu Nawe, Ee Mungu wangu!} x2