Indirimbo Zikundwa Open in the app

#87

Nakaza mwendo mbinguni kila siku

Izindi

Couplet 1

Nakaza mwendo Mbinguni, kila siku napanda juu naomba nikisafiri, “Bwana Uniongoze juu. ”

Refrain

Bwana uniinue juu kwa Imani hata Mbingu; Juu kuliko dunia Bwana Uniongoze juu.

Couplet 2

Moyo wangu hautaki kukaa palipo shaka wengine wapenda chini nia yangu ni kupanda.

Refrain

Bwana uniinue juu kwa Imani hata Mbingu; Juu kuliko dunia Bwana Uniongoze juu.

Couplet 3

Nataka kupanda juu nisishindwe na adui kwa Imani nasikia sauti ya washindaji.

Refrain

Bwana uniinue juu kwa Imani hata Mbingu; Juu kuliko dunia Bwana Uniongoze juu.

Couplet 4

Kupanda juu nataka niuone Utukufu hata mwisho nitaomba, “Bwana Uniongoze juu.”

Refrain

Bwana uniinue juu kwa Imani hata Mbingu; Juu kuliko dunia Bwana Uniongoze juu.