#80
Twasoma ni njema sana mbinguni
Izindi
Couplet 1
Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; Twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, Vinanda vizuri viko, Na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana.
Couplet 2
Siku zote ni mchana, ni Nchi ya raha; Wala machozi hapana, ni Nchi ya raha; Walioko wanuona Uso wa Mwokozi, tena Jua jingine hapana, ni Nchi ya raha.
Couplet 3
Nyama na vitu viovu havimo kabisa; Kifo nacho, na ubovu, havimo kabisa. Ni watakatifu wote, wameoshwa dhambi zote; Wasiosafiwa wote hawamo kabisa.
Couplet 4
Tuna dhambi, pia sote, Mwokozi akafa; Kwake tutaoshwa zote, Mwokozi akafa; Kwake twapata Wokovu, tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa.
Couplet 5
Baba, mama, ndugu zetu, twendeni kwa Bwana; Huku chini sio kwetu, twendeni kwa Bwana; Tusishikwe na dunia, na dhambi kutulemea; Tutupe vya chini pia, twendeni kwa Bwana.