#54
N.m 315 nimepata salama kutoka mbinguni
Izindi
Couplet 1
Nimepata Salama kutoka Mbinguni, sasa ninapumzika kwa Yesu. Na katika mateso na taabu za hapa ninaona Salama na kimya.
Refrain
Nimepata Salama, ni Salama kutoka Mbinguni; ni Salama ya Mungu kulinda mioyo; Ndiyo inayopita kusema.
Couplet 2
Sina mali nyingine kupita Salama Mungu aliyoleta kwa mimi; na Salama hii mtu hawezi kutoa itakuwa milele moyoni.
Refrain
Nimepata Salama, ni Salama kutoka Mbinguni; ni Salama ya Mungu kulinda mioyo; Ndiyo inayopita kusema.
Couplet 3
Sasa ninapumzika katika Salama kwa mikono ya Yesu Mwokozi; Ninalala usiku pahali popote; Bila woga wa kitu chochote.
Refrain
Nimepata Salama, ni Salama kutoka Mbinguni; ni Salama ya Mungu kulinda mioyo; Ndiyo inayopita kusema.
Couplet 4
Na wakati nitakapofika Mbinguni, Nitaona Mwokozi Mpenzi nitapiga Asante kwaye kwa Salama iliyonituliza saa zote.