Indirimbo Zikundwa Open in the app

#117

Ndugu musikiye

Iz'i Gisenyi

Couplet 1

Ndugu musikiye ginsi Bwana Yesu alivyotumika hapa duniani alikuwa Baba Muumba wa vyote akageuka Mwana akageuka Roho.

Refrain

Agano lakale aliitwa Baba Muumba wavyote muweza wa vyote agano la sasa ni Mwokozi wetu Mfalme wetu kiongozi chetu.

Couplet 2

Alikuwa Baba Muumba wa vyote mwanzo wa vyote mwisho wavyote akageuka Mwana Mukombozi wetu akageuka Roho mufariji wetu.

Refrain

Agano lakale aliitwa Baba Muumba wavyote muweza wa vyote agano la sasa ni Mwokozi wetu Mfalme wetu kiongozi chetu.

Couplet 3

Baba siyo jina Mwana siyo jina Roho siyo jina, Jina ni Yesu, Yesu ndiye Baba ,Yesu ndiye Mwana, Yesu ndiye Roho Alfa na Omega.

Refrain

Agano lakale aliitwa Baba Muumba wavyote muweza wa vyote agano la sasa ni Mwokozi wetu Mfalme wetu kiongozi chetu.

Couplet 4

Sasa wewe ndugu ubatizo gani uliobatizwa ulipo amini, amini Bwana YESU ukabatizwe katika Jina lake uhai.

Refrain

Agano lakale aliitwa Baba Muumba wavyote muweza wa vyote agano la sasa ni Mwokozi wetu Mfalme wetu kiongozi chetu.

Couplet 5

Maana yake Yesu, Yesu ni Mwokozi mweye ufufuko na uzima kila amwaminie Yesu wa uzima hata akifa atafufuka.