Indirimbo Zikundwa Open in the app

#612

Njoni mwenye dhambi

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Njoni! Njoni! Wenye dhambi, Njoni, msikawie; Yesu Anawangojea, Ndiye Awapendaye; Ajuaye Awezaye Kuwaponya ni Yeye.

Couplet 2

Ewe muhitaji uje; Anakukaribisha; Imani, kweli na toba, Neema ya kutosha, Jua sana, Kwake Bwana bure utayapata.

Couplet 3

Njoni, mlio lemewa Na dhambi ya Adamu; Mkingoja kujiponya Mtapotea mumu; Si wa haki, ni wakosa Waoshwao kwa damu.

Couplet 4

Ikamtokea dhiki, Mle Gethisemani; Kisha Alipoangikwa Akalia Mtini: “Imekwisha”, Alitosha Dhabihu ya thamani.

Couplet 5

Kristo Aliye Mbinguni Hutuombea huko; Basi mtumai Yeye; Kamwe mwingine hako, Yesu peke’, Yesu peke’, Ndiye Mwokozi wako.

Couplet 6

Wamsifu-sifu sana Mbinguni Malaika; Wachanganya Nyimbo zao Na waliookoka: Aleluya Wataimba Waliooshwa taka.