Indirimbo Zikundwa Open in the app

#432

Yesu Kristo aliacha sifa

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Yesu Kristo aliacha Sifa zake zote Mbinguni, Katika Bethelehemu Alizaliwa kama m-tu, Sasa tumwimbie sana, Tumshukuru kwa furaha, Ndiye Mfalme wa wafalme Jana, leo hata milele.

Couplet 2

Alitembelea pote, Akafanya kazi kwa nguvu, Alipenda wanadamu Na kuwaokoa wagonjwa, Alizifukuza pepo, Akawafufua wafu, Wale vilema, vipofu, Aliwahurumia wote.

Couplet 3

Alisulibishwa bila Kufanya ubaya wo wote, Makuhani na waandishi Kwa uongo walimfitini, Alisema, « Imekwisha », Jua lilikuwa giza, Kaburini alizikwa, Wengi wafufuke rohoni.

Couplet 4

Katika siku ya tatu Alitoka mzima kwa wafu, Akawatokea wengi, Akachukuliwa Mbinguni, Atarudi kututwa-a, Kwa hiyo tukae macho, Siku zote tumwimbie, Ndiye Mfalme wetu milele.