#425
Taraja yangu
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Sina nguvu ya kutimiza Sheria Yako, mapenzi Yako; Lakini najua tu kitu moja, Neema Yako ni kubwa kwangu. Mukosefu, muzaifu, Maisha yangu ni muregevu; Lakini najua tu kitu moja, Damu Yako ndjo taraja yangu.
Refrain
Damu yako ndjo taraja yangu, Kalvari ndjo taraja yangu, Golgotha ndjo taraja yangu, Mateso yako ndjo taraja yangu.
Couplet 2
Roho yangu inahuzunika Kwa mwenendo wangu hapa dunia; Lakini najua tu kitu moja: Damu Yako ndjo uficho wangu. Ulipanda kule Mbinguni, Siku kwa siku unaniombea Na kunikankamisha kila siku, Na kunifariji ndani ya mateso.
Refrain
Damu yako ndjo taraja yangu, Kalvari ndjo taraja yangu, Golgotha ndjo taraja yangu, Mateso yako ndjo taraja yangu.
Couplet 3
Roho yangu, mawazo yangu, Maisha yangu ni Wewe Yesu, Sababu ulilaka kitu moja, Kwa kunichukua na kwenda Nawe. Mufariji, Mukombozi, Mutunzaji ni Wewe Yesu, Ninategemea kurudi Kwako Na kuishi Nawe kwa milele.
Refrain
Damu yako ndjo taraja yangu, Kalvari ndjo taraja yangu, Golgotha ndjo taraja yangu, Mateso yako ndjo taraja yangu.