Indirimbo Zikundwa Open in the app

#413

Vita itakapokuisha

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Vita itakapokwisha, Na kazi zetu huku; Tutapewa pumziko Mbinguni milele.

Refrain

Mji nzuri wa furaha, Pumziko la milele, Bila shida na usiku, Yesu pekee ndiye Nuru; Kwa imani toka mbali, Huku chini twatazama Mji mzuri sana, Makao ya wateule.

Couplet 2

Kweli kuna pumziko Kwa wana Wake Mungu; Maombolezo na taabu Yote itakwisha.

Refrain

Mji nzuri wa furaha, Pumziko la milele, Bila shida na usiku, Yesu pekee ndiye Nuru; Kwa imani toka mbali, Huku chini twatazama Mji mzuri sana, Makao ya wateule.

Couplet 3

Siku njema ya Furaha Yakaribia sana; Tumtegemee Bwana, Tumwamini kweli.