Indirimbo Zikundwa Open in the app

#390

Tuna makao mbinguni

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Tuna makao Mbinguni, Alivyosema Bwana, Anatutengenezea Sisi tumwaminio. Sasa wakati wa giza Tungali tu maskini, Kesho tutakwenda Kwake, Tutajirike huko.

Refrain

Kwake Yesu, tuwe pamoja Naye, (Furaha kuu) ndivyo tutafurahi milele.

Couplet 2

Sasa katika mateso Nayo huzuni yote, Tuzidi kumtegemea Bwana Mwokozi wetu. Nuru yafukuza giza, Tukae kwa salama, Bwana anatungojea Kwake kule Mbinguni.

Refrain

Kwake Yesu, tuwe pamoja Naye, (Furaha kuu) ndivyo tutafurahi milele.

Couplet 3

Atarejea Mwokozi, Kazi itakomeshwa, Siku inakaribia Ndiyo tunangojea; Kwa hiyo tukae macho, Atakaporejea, Atatukuta tayari Kwenda naye Mbinguni.

Refrain

Kwake Yesu, tuwe pamoja Naye, (Furaha kuu) ndivyo tutafurahi milele.