#346
Yerusalema mupia
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Niliona Yerusalema mpya Ikishuka toka Mbingu kwa Baba. Imepambwa sawa Bibi Arusi Mwenye furaha juu ya Mume Wake. (x2)
Couplet 2
Neno kubwa toka Mbingu kwa Baba Ikisema: tazama neema ya Mungu Ni pamoja na watakatifu, Atakuwa pamoja na wao. (x2)
Couplet 3
Bwana Yesu Yeye ni tayari Kwa kuchukua Bibi Arusi, Juu ya ndoa yake kule Mbingu Kutakuwa furaha ya milele. (x2)
Couplet 4
Na mauti haitakuwa tena Na vilio vyote na uchungu, Na giza haitakuwa tena Kwani nuru ni Mwana Kondoo. (x2)
Couplet 5
Ndugu na dada, tuwe tayari, Bwana Yesu Yeye alisema: « Nitarudi mufano wa mwizi ». Hatujui siku atarudi. (x2)
Couplet 6
Majivuno haitakuwa tena, Mazehebu yote itapita, Vya dunia vyote vitapita; Neno Lake haitapita kamwe. (x2)