Indirimbo Zikundwa Open in the app

#329B

Siku ya mbingu kujawa

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Siku ya Mbingu kujawa na sifa, Dhambi zilizidi duniani; Yesu akaja azaliwe mtu, Awe na watu ulimwenguni.

Refrain

Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.

Couplet 2

Na siku moja walikwenda naye, Wakamkaza Msalabani; Aliumia, aliaibishwa, Ili atuokowe dhambini.

Refrain

Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.

Couplet 3

Siku hiyo wakamlaza chini Kaburini alipumzika; Matumaini yetu wenye dhambi, Ni Mwokozi, kwake twaokoka.

Refrain

Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.

Couplet 4

Kaburi likashindwa kumshika; Jiwe likatoka mlangoni, Alifufuka kwa kushinda kwake, Naye yuko milele Mbinguni.

Refrain

Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.

Couplet 5

Siku moja atatujia tena; Utukufu wake tutaona; Atawaleta na wapenzi wetu; Mwokozi wangu, tutaonana.