#313
Umesikia kisa
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Umesikia kisa cha Mwana wa Betelehemu: Malaika, wa akili walimwabudu Yeye; Alifundisha waalimu Ekaluni mwa Mungu, Nafurahi kukuambia na leo Yuko sawa.
Refrain
Na leo Yuko sawa, na leo Yuko sawa, Kuita wapotevu, hata awaponyeshe; Aksante Yuko sawa sawa.
Couplet 2
Umesikia kisa sawa alivyotembea Kwendea mitume mawimbini pa Galilaya; Na mufano mawimbi yalitii amri Zake, Nafurahi kukuambia na leo Yuko sawa.
Refrain
Na leo Yuko sawa, na leo Yuko sawa, Kuita wapotevu, hata awaponyeshe; Aksante Yuko sawa sawa.
Couplet 3
Umesikia viwete, vipofu vya zamani, Wagonjwa wa kila ginsi waliponywa kabisa; Pepo ziliondolewa, ukoma wasafishwa, Yesu mo Muganga kubwa na leo Yuko sawa.
Refrain
Na leo Yuko sawa, na leo Yuko sawa, Kuita wapotevu, hata awaponyeshe; Aksante Yuko sawa sawa.
Couplet 4
Umesikia Yesu akiomba Getsemane Na ginsi alipokufa juu ya Musalaba Kichwa kilitobolewa na kofia ya miiba Kwa ajili yako ndugu, na leo Yuko sawa.
Refrain
Na leo Yuko sawa, na leo Yuko sawa, Kuita wapotevu, hata awaponyeshe; Aksante Yuko sawa sawa.
Couplet 5
Anayestahili shangwe, Mungu mukamilifu, Kumwabudu Yeye Bwana Mufalme wa wafalme; Asifiwe, asifiwe, Yehova Mungu wetu! Leo na milele sisi tutamwabudu Kristo.
Refrain
Na leo Yuko sawa, na leo Yuko sawa, Kuita wapotevu, hata awaponyeshe; Aksante Yuko sawa sawa.