#304
Mabawani mwake
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Mabawani Mwake niko salama, Hata giza na zoruba nguvu; Nina amini Muchungaji wangu, Amenikomboa, niko Wake.
Refrain
Mabawani, mabawani, Nani atatutenga? Mabawani atanichunga, Nitachungwa Salama.
Couplet 2
Mabawani Mwake ninajificha, Hamu ya roho kupumzika, Sina wakuniponya duniani, Napata faraja na baraka.
Refrain
Mabawani, mabawani, Nani atatutenga? Mabawani atanichunga, Nitachungwa Salama.
Couplet 3
Mabawani Mwake ninafurahi, Mule nitaepuka mabaya; Nafichwa, nakingwa na ninalindwa, KatikaYesu niko Salama.
Refrain
Mabawani, mabawani, Nani atatutenga? Mabawani atanichunga, Nitachungwa Salama.