#263
Ninakukaribia, ee bwana
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Ninakukaribia, ee Bwana wa mapendo, Unisamehe leo makosa yangu yote; Neema yako Bwana nayahitaji sana, {Katika mwendo wangu kufika kule kwako.} x2
Couplet 2
Hata adui zote wanasimama hapa, Sitaogopa tena kwa Jina lako Yesu, Sababu ulishinda mauti na kaburi; {Na deni yangu yote ilisha malizika} x2
Couplet 3
Kwa Jina lako Yesu nitayaona Mbingu, Sitapotea tena, aksante Bwana wangu. Neema kubwa gani ulionyesha kwangu: {Kunitosha kwa zambi kusudi niwe wako} x2
Couplet 4
Pokea shukrani, ee Bwana, kule Mbingu, Tokea wana wako uliowakomboa; Kwa neema yako Bwana, tutariti na Wewe {Hivi unastahili utukufu milele} x2