Indirimbo Zikundwa Open in the app

#256A

Wanatoka dhambini

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Wanatoka dhambini na dhikini, Wanaokolewa; Wanakwenda kwa Yesu na furaha, Kwake Yesu! Anatutengenezea makao, Tutakuta amemaliza yote, Tutapata mavazi meupe mno, Tutakaa pamoja naye Yesu.

Refrain

Nyumbani Mbinguni Wataingia Wakristo tu, Kumwona Mwokozi kwa Furaha.

Couplet 2

Tutafurahi pamoja na wengi Wakristo Mbinguni, Kazi zetu tutakapomaliza, Tupumzike! Maji yaliyo hai ni mengi mno, Hatutaona kiu siku zote, Tutakunywa kwa furaha milele, Mbele yake Mwokozi wetu Yesu.

Refrain

Nyumbani Mbinguni Wataingia Wakristo tu, Kumwona Mwokozi kwa Furaha.

Couplet 3

Bwana Yesu, tunakutumaini Milele Mbinguni; Tutafurahi kukuona Wewe, Tukusifu! Vitakwisha huzuni na mauti Vinavyotusumbua siku hizi, Dhambi nazo Bwana utaondoa, Tuwe nao uzima wa milele.

Refrain

Nyumbani Mbinguni Wataingia Wakristo tu, Kumwona Mwokozi kwa Furaha.