Indirimbo Zikundwa Open in the app

#181A

Ni salama rohoni

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu.

Refrain

{Salama rohoni,} x2 Ni salama rohoni mwangu.

Couplet 2

Ingawa Shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwami Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.

Refrain

{Salama rohoni,} x2 Ni salama rohoni mwangu.

Couplet 3

Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukuwi laana yake, Ni salama rohoni mwangu.

Refrain

{Salama rohoni,} x2 Ni salama rohoni mwangu.

Couplet 4

Ee Bwana imiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa- Ni salama rohoni mwangu.

Refrain

{Salama rohoni,} x2 Ni salama rohoni mwangu.