#119
Nitawaambia ushuhuda
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Nitawaambia ushuhuda wangu, Yesu a’okoa. Nilikuwa mbaya, nilikuwa mbali, Yesu ‘kaniita.
Refrain
Yote ni mapia (machoni mwangu), Yote ni mapia (rohoni mwangu), Yote ni mapia (katika Yesu), Nimekombozwa toka zambi. (x2) (mimi).
Couplet 2
Niliteta mimi, niliiba mimi, Yesu ni M’kuu; Nilipiga watu na kuwatukana Yeye ‘kaniita.
Refrain
Yote ni mapia (machoni mwangu), Yote ni mapia (rohoni mwangu), Yote ni mapia (katika Yesu), Nimekombozwa toka zambi. (x2) (mimi).
Couplet 3
Nayo mapia yangu, nimekombolewa Toka utumwani; Sasa macho yangu yametiwa nuru, Yesu asifiwe!